Stop masturbation
you will die barren
Kujichua ni tabia ya kingono ambayo inapofanywa kwa kiwango kikubwa inaleta matatizo ya kiumbo na kisaikolojia kwa anayefanya tendo hilo.
Kujichua ni tabia ya kingono ambayo inapofanywa kwa kiwango kikubwa inaleta matatizo ya kiumbo na kisaikolojia kwa anayefanya tendo hilo.
Na katika kipindi cha zama hizi ambazo majarida, vipindi na hata
mitandao mingi inaonyesha picha za ngono ndio kunaifanya tabia hii kushamiri
kwa kiwango kikubwa.
Kwani vijana wengi wanaingia katika mchezo huu wa kujiridhisha
wenyewe bila kujua madhara yatakayokuja baadaye.
Waelimisha rika wengi wamekuwa wakiwaambia vijana kwamba kujichua
ndio njia salama ya ngono kwani hatari ya kupata magonjwa kwako haipo na
wanaongezea kuwa wafanye kwa kiwango kidogo pale wanapojisikia hamu ya tendo.
Lakini wanasahau kuwaeleza madhara yake pindi inapofanywa kwa
kiwango kikubwa na pia wanajua wazi kuwa mara mtu anapoanza tabia hii kuitawala
kwa
Baadhi ya madhara ambayo unaweza ukayapata ukifanya kwa muda
mrefu:
1.Maumivu ya mgongo kwa chini;
2.Kupoteza nywele;
3.Kupungua nguvu za kiume;
4.Kuwahi kumaliza wakati wa tendo;
5.Kupoteza uwezo wa kuona vizuri;
6.Maumivu ya kende;
7.Maumivu ya nyonga;
8.Kuchoka sana;
9.Msongo wa mawazo;
10.Kupoteza kumbukumbu kwa haraka
Dhumuni la makala hii ni kumsaidia yule mtu ambaye tayari anafanya
mchezo huu atambue madhara yake na pia afahamu namna ya kujinasua kabla mambo
hayajawa mabaya.
Kwa wewe muhusika unatakiwa kuwa na hakika kuwa unaweza ukajinasua
katika tatizo lako hili.
Wengi wanaume kwa wanawake waliojaribu kujisaidia kuondokana na
hili tatizo wameweza, hata wewe kwako ni hivyo hivyo ikiwa utajitambua
tu.
Kujitambua ni hatua ya kwanza katika safari yako ya kuacha.
Unatakiwa uamue kuwa sasa unaacha na pindi unapoweka uamuzi huo
utakuwa unasaidia kujipunguzia ukubwa wa tatizo.
Lakini inatakiwa uwe na zaidi ya tumaini au tamanio la kutambua
kuwa uamuzi wa kuacha ni muhimu kwako.
Ni uamuzi tu.
Ukiweka kweli kabisa mawazo yako katika kuliondoa hili tatizo
utakuwa na nguvu ya kuweza kuliondoa kabisa na kujiweka pembeni na vishawishi
vya kukurudisha katika hiyo tabia.
Utakapo kuwa ushafanya uamuzi wa kuacha anza kufanya yafuatayo:
1.Usiguse wala kuchezea maeneo yako ya siri kwa muda mrefu labda
uwe unajisafisha wakati wa kuoga.
2.Tengana na rafiki au marafiki zako ambao unajua wazi kabisa kuwa
nao wana tabia hizo kwani usijidanganye kuwa mtaacha wote kwa pamoja kwani mara
nyingi kuacha ni juhudi na maamuzi binafsi.
3.Unapokuwa unaoga usikae muda mrefu maeneo hayo jifute na utoke haraka.
4.Lala na nguo inayozifunika sehemu za siri kiasi kwamba sio
rahisi kwa wewe kuzigusa mpaka uivue hiyo nguo, hapa itakusaidia kupata muda wa
kutafakari kabla hujafanya tendo lolote.
5.Endapo upo kitandani na mawazo ya tendo hilo yakakujia ,nyanyuka
na ujaribu kutembea tembea ili kuyapoteza hayo mawazo kichwani mwako.
6.Usisome majarida ya ngono, na kuangalia picha za ngono kwani
vitakuchochea urudi katika tatizo.
7.Anza kusoma majarida na makala za mambo mazuri na yenye
kuelimisha na itakusaidia kuulisha ubongo taarifa nzuri.
Mathalani unaweza ukaanza tabia ya kusoma vitabu vya dini
itakuasidia sana.
8.Sali, lakini wakati wa kusali usiwe mara kwa mara unalifikiria
hili tatizo kwani utaendelea kuliweka mawazoni mwako.
Mtazamo wa mtu mwenyewe ndio unaosaidia kuliondoa hili tatizo kwa
haraka.
Ukiweza kutambua kwanini umeingia katika hii tabia,
na kuyafahamu mazingira yanayokuchochea wewe kuingia huko
unatengeneza uwezo wa kuishinda kwa haraka.
Tabia hii ya kujiridhisha mwenyewe itakufanya uwe mtu kwa
kujisikia na hatia kila mara, kutojiheshimu mwenyewe na kukufanya uendelee
pindi unapopatwa na msongo wa mawazo.
Na inapelekea unaanza kujiona mdhambi hata kuhudhuria nyumba za
ibada kwako inakuwa ngumu.
UAMUZI WA KUACHA UNAWEZA KUUFANYA SASA
KWAAJILI YA AFYA YAKO YA UZAZI NA AKILI.
ANZA JUHUDI NA UTAONA JINSI UNAVYOWEZA KUISHI BILA TABIA HIYO
AMBAYO HAINA FAIDA YOYOTE SIKU ZA BAADAYE.
No comments:
Post a Comment