“HUU NDIO UJASIRIAMALI”
USISHINDWE KUANZISHA BIASHARA KWA KUKOSA MAARIFA!
“ili ndoto yako itimie”
“ili ndoto yako itimie”
Benki ya Azania inakusudia kuwa benki inayoongoza katika kutoa huduma za kibenki |
kwa wateja wadogo
na wa kati.
Hatua muhimu za kuzingatia!
1. Nyambulisha na uainishe mradi
unaotaka kufanya kwa msingi wa wazo
linalotekelezeka
2. Fursa
ya biashara hutokana na yafuatayo
a. Tathmini ya wazo lako la biashara.
b. Tathmini ya kina ya mahitaji
ya soko ambalo biashara yako italenga.
c. Tathmini ya kina ya bidhaa zako na huduma zako.
d. Tathmini ya kina na jinsi bidhaa yako/huduma yako itakavyokidhi mahitaji ya soko ulilolenga
e. Fikiria na ufafanue walengwa/watumiaji wa bidhaa au huduma zako.
f. Tathimini
taratibu za kisheria na kiutawala
kuhusu biashara
unayotaka kuanzisha.
3. Angalia ushindani uliopo
sokoni (husisha yafuatayo)
a. Angalia na uorodheshe
biashara
nyingine zinazotoa huduma/bidhaa kama unazotaka kutoa
wewe.
b. Angalia na ujiulize kama wapo washindani wengine
wapya wanaotaka kuingia kwenye
biashara hiyo hiyo unayokusudia.
c. Jiulize changamoto zilizopo na vikwazo vilivyopo (kisheria, kimtaji, au vinginevyo) vinavyoweza kuzuia biashara nyingine zinazofanana na biashara yako kuanzishwa.
d. Jiulize na uorodheshe upekee wa bidhaa/huduma zako (jiulize sababu za kumfanya mtu ahitaji bidhaa/huduma yako badala ya bidhaa/huduma nyingine
zilizopo sokoni)
4. Angalia uwezekano wa biashara yako kuendelea na kukua
(ujibu yafuatayo)
a. Utawafikiaje
walengwa wa biashara yako (Ni
kwa vipi walengwa
wako watajua kuhusu bidhaa na huduma zako)?
b. Utasambazaje/ fikishaje bidhaa/huduma zako (Bidhaa zako zitafikaje
kwa wauzaji wa rejareja au huduma zako zitafikaje
kwenye maeneo uliyokusudia
na
maeneo hayo ni yapi)?
c. Nini makadirio yako ya wafanyakazi unaohitaji
kwa miaka miwili ya kazi (wafanyakazi
wangapi utahitaji mwaka wa kwanza, na wangapi utahitaji
mwaka wa pili)?
d. Unahitaji ufanye nini ili biashara yako ipate faida na itachukua
muda gani kuwa na faida?
e. Nini matarajio yako ya mapato na matumizi kwa miaka 4 ya kazi (ni mapato na matumizi kiasi gani katika mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, wa tatu na wa nne)?
f. Unahitaji mtaji wa kiasi gani (kiasi gani cha fedha unachohitaji kuwekeza) katika mwaka wa kwanza,wa pili, wa tatu na wa nne ili kuendesha biashara
yako?
g. Utawezaje kupata kiasi hicho cha mtaji? Je ni kwa kuanza kuweka akiba katika benki au kuomba mkopo na kwa gharama gani?. Je mchango wako katika mtaji ni kiasi gani?
h. Je mradi wako unaweza ukabeba gharama zinazotakiwa kiundeshaji na bado ukazalisha faida?
5. Uzoefu
wako katika
ujasiriamali na uwajibikaji.
a. Tathmini kiwango chako cha elimu na uzoefu wako unaohusiana na wazo lako la biashara
na mahusiano uliyo nayo na wadau muhimu ki- sekta wewe kama mjasiriamali.
b. Tathmini kuhusu wataalam
wa fani mbalimbali ambao utahitaji kuwatumia katika maeneo ambayo wewe si mtaalam wala mzoefu ili kufanikisha
uanzishaji na uendeshaji
wa biashara yako.
c. Kwa ufupi tathmini
nia/malengo yako ya kutimiliza kuanza na kukua kwa biashara ukizingatia muda utakaotumia kupanga, muda unaokusudia
kutumia katika mradi, kiwango cha fedha za kwako mwenyewe
unachoridhia kuweka katika mradi n.k.
Z I N G A T I A H A Y A A N D A A T U O N E
ili ndoto yako ya kumiliki na kuendesha biashara endelevu itimie
Azania Bank Limited Masdo House Samora Avenue
Box 9271Dar es Salaam,
Tanzania
Tel: 255 22 2118014, 2117998 -
9, 2118025 - 6
Fax 255 22 2118010 -
1 www.azaniabank.co.tz
No comments:
Post a Comment