UNADHANI KITU GANI NI KIGUMU ZAIDI KUWA
MTENDAJI MKUU?
Hapa jikite zaidi katika mipango, utekelezaji, na gharama za
usimamizi.
Elezea kuwa kazi kubwa kwa mtendaji mkuu ni kuwafanya wafanyakazi
wake kufanya kazi kulingana na mipango ya ofisi, kuitekeleza kazi hiyo katika
muda uliopangwa na pia ikamilike ikiwa imetumia bajeti iliyopangwa.
17.UNAUONAJE MWENENDO WA SOKO LA SHUGHULI ZETU?
Jiandae na vitu viwili au vitatu kuhusiana na mwenendo wa soko, na
uonyeshe jinsi gani unalifahamu soko vizuri.
Unaweza ukagusia suala la changamoto za teknolojia au fursa, hali
ya uchumi na hata mahitaji ya mamlaka zinazosimamia soko ili kuonyesha ni wapi
soko la shughuli zenu linapoelekea.
18.SABABU GANI ZIMEKUFANYA UIACHE KAZI YAKO NA
KUJA KUTAFUTA MPYA?
Elezea kwa kifupi sababu zako, kuwa mwaminifu pia bila kujiumiza
wewe mwenyewe.
Waeleze kuwa kuondoka huko ulikuwa ni uamuzi wako, na wewe ni mtu
wa kupenda kutafuta changamoto mpya na umeona sehemu sahihi ya wewe kuzipata ni
hapa kwao.
Usije ukaelezea matatizo yako binafsi hapa, kwani unaweza
ukajiharibia. Wanacholenga wasaili katika hili swali ni kujua kama ulifukzwa au
uliondoka mwenyewe.
19.UMEJISIKIAJE KUACHA FAIDA ZA MAKATO YAKO KWA
KUACHA KAZI ULIKOTOKA?
Waambie kuwa kiuhalisia uliguswa, lakini hukuwa na hofu.
Waambie kwamba ulikuwa tayari kuacha faida zote ili ukapate
mazingira sahihi ya kazi ili uonyeshe kuwa maslahi si kipaumbele cha wewe
kuajiliwa na wao.
20.KITU GANI ULIKUWA UNAKIPENDA, NA ULICHOKUWA
UKIPENDI KATIKA KAZI YAKO ILIYOPITA?
Kuwa mwangalifu wakati wa kujibu hili swali, uwe na mtazamo chanya
zaidi kwa kuelezea vitu vingi ulivyokuwa unavipenda kuliko ulivyokuwa
unachukia.
Ukijifanya unataka kukosoa sana kazi uliyokuwa unafanya kabla ya
kuja kuomba kwao, itawashangaza na kukuuliza kwanini uliendelea kubaki mpaka
leo ndio uje kwao?
21.ULIKUWA UNAMUONAJE MKUU WAKO WA KAZI?
Hapa pia kuwa na mtazamo chanya, kwani hata kama mkuu wako hakuwa
mwema kwako,
ila jinsi utakavyomzungumzia kwa kuponda ndivyo muajili wako
mpya atahisi utamfanyia yeye siku zijazo.
22.KWANINI UNAHISI HAUJAVUNA SANA KATIKA UMRI
WAKO HUU?
Hapa waambie sababu moja kuu, ya kuwa ndio maana umekuja kwao
kutafuta kazi
na kuwa unajua thamani yako itapanda kupitia wao.
Usianze kujitetea sana hapa mpaka ukawaonyesha kuwa huna mipango
mizuri na maisha yako.
23.UNADHANI KWA NAFASI UNAYOOMBA ULIPWE KIASI
GANI?
Huu ni mtego mkubwa sana kwa wewe unayeomba kazi, unatakiwa uwe
unafahamu viwango vya mishahara ya majukumu kama yako.
Endapo huyajui majukumu ya kazi yako, unaweza ukawauliza hapo hapo
ili ukishayafahamu ndio uwatajie kiwango unachotaka.
Usije kujirahisisha au kujipandisha sana hapa, kwani nao
wanaangalia kama uko kimaslahi zaidi kuliko majukumu utakayopewa.
Au kuwatega na wewe, kama uliacha ajira mahali unaweza ukawaambia
kuwa ulikotoka ulikuwa unalipwa kiasi fulani na ungependa kuona kiwango
kinapanda.
24.UNA MIPANGO GANI YAKO YA MUDA MREFU?
Hapa wala usijisumbue na maelezo mengi, gusia kwa kifupi malengo
yako ukiyahusianisha na malengo ya kampuni unayoomba.
25.UMEFANIKIWA KWA KIASI GANI MPAKA SASA?
Waeleze kuwa unajivunia na jinsi ujuzi wako unavyokua siku hadi
siku.
Waambie pamoja na changamoto za kupanda na kushuka katika maisha
lakini huna malalamiko na hatua uliyopo.
Hapa jionyeshe ni jinsi gani unajiamini na unafurahia unachofanya
katika maisha yako.
HAYA NDIO MASWALI KUMI YALIYOKUWA YAMEBAKI
AMBAYO NDIO HUWA YANAPENDWA KUULIZWA SANA WAKATI WA USAILI.
YAWEZEKANA KUNA MENGINE MENGI MAPYA UTAKUTANA
NAYO LAKINI UNACHOPASWA KUFANYA NI KUJIANDAA KWA KUTUMIA PICHA ULIYOPATA KUTOKA
KATIKA HAYA MACHACHE YA MIFANO.
No comments:
Post a Comment