Majukumu ya Idara kwa Ujumla
Majukumu ya Idara
Upimaji na Ramani ni Idara katika
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi. Jukumu lake kubwa ni usimamizi wa
upimaji ardhi na utayarishaji wa ramani na plani mbalimbali za nchi mijini na
vijijini. Ramani hizo ni msingi wa kubuni, kutekeleza na kuratibu mipango ya
maendeleo juu ya ardhi katika sekta na kwa matumizi mbalimbali kama:
- Umilikishaji ardhi
- Kupanga matumizi ya ardhi
- Utalii
- Mawasiliano
- Makazi
- Kilimo
- Hifadhi ya mazingira
- Utafiti na uchimbaji madini
2. Bidhaa zinazouzwa
Urasimu ramani
|
2.1 Ramani.
Ramani za
msingi kutokana na picha za anga (base maps):
- Ramani za topografia za skeli ya kati 1:50,000 kwa nchi nzima
- Ramani za maeneo ya mijini katika skeli ya 1:2,500 au 1:5,000
Ramani za kuzalisha kutokana na
ramani za msingi
- Ramani katika skeli ya1:250,000
- Ramani za Mikoa na Wilaya katika skeli kati ya 1:300,000 -1:500,000
- Ramani za masomo maalum
- Ramani ya Barabara ya Tanzania katika skeli 1:2m
- Ramani yaTawala za Mikoa na Wilaya katika skeli ya l:2m
- Ramani ya Jiji la Dar es Salaam katika skeli ya I :20,000
- Ramani ya Utalii ya Mlima Kilimanjarokatikaskeli ya 1:1 00,000
2.2 Picha za Anga
Idara ya upimaji na ramani ina
maktaba ya picha za anga za sehemu mbalimbali za nchi zilizopigwa
katika nyakati mbalimbali tangu miaka ya
1940.
- Picha za ,skeli ndogo chini ya 1:50,000
- Picha za skeli ya kati I :20,000 1:50,000
- Picha za skeli kubwa zaidi ya 1:20,000
2.3 Takwimu na kumbukumbu za
Upimaji Ardhi.
Idara ni mhazini wa
takwimu na kumbukumbu za upimaji
miliki nchini
- Kadi za vielelezo vya alama za msingi za upimaji
- Vipimo vya alama za msingi za upimaji
- Plani za upimaji miliki
2.4 Bidhaa Maalum
Idara
ina uwezo kivifaa na
kitaaluma kutayarisha ramani, na kutoa huduma
mbalimbali kukidhi mahitaji ya wateja
- Ramani maalum, kulingana na ubunifu na vigezo vya mteja
- Picha-ramani (orthophoto)
- Muunganisho wa picha nyingi kuwa moja.
- Ramani katika mfumo wa kompyuta
- Ramani ya awali iliyochorwa kwa mashine za photogrammetry Kumbukumbu Kuu ya Uoto kwa nchi nzima(katika mfumo wa kompyuta)
- Picha za anga katika mfumo wa kompyuta kwa baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam
3.0 Huduma Mbalimbali
3.1 Upimaji
Idara
ina uwezo kivifaa na
kitaaluma kufanya upimaji wa aina mbalimbali
- Upimaji miliki ukubwa wowote mahali popote nchini
- Upimaji wa kuweka mifumo ya alama za msingi za upimaji
- Upimaji kwa ajili ya utayarishaji wa ramani kutokana na picha za anga
- Upimaji kwa kazi za uhandisi kama vile:
- Miinuko na ubapa wa barabara
- Mapito ya njia za mawasiliano
3.2 Uchoraji na Uchapaji wa
Ramani
- Tafsiri na utambuzi wa alama katika picha kwa madhumuni ya kuchora ramani, matumizi ya ardhi ama uoto juu-yake.
- Uchoraji kwa mitambo ya photogrammetry
- Usanifu wa ramani
- Utoaji nakala za ramani au plani katika filamu kwa kamera maalum
- Ukuzaji wa nyaraka kwa njia ya kamera hadi x6
- Kushona vitabu
Uchapaji ramani
- Kuchapa ramani katika rangi nyingi au moja hadi ukubwa wa 30" X 40"
3.3 Uwezo wa Kupima na Kuchora
Ramani kwa Teknolojia ya Kompyuta.
- Uchoraji wa ramani kwa kutumia mashine za photogmmmetry zilizoshikizwa na kompyuta
- Uingizaji wa ramani katika kompyuta kwa njia ya board or screen digitization hadi ukubwa wa AO
- Upimaji ardhi kwa kutumia kifaa cha Total Station ambacho hunasa vipimo na takwimu moja kwa moja katika mfumo wa kompyuta
- Upimaji kwa taaluma ya anga za juu GPS
- Kupata ramani ya umbile la ardhi kuonyesha mwinuko na mabonde usawa wa bahari
- Upimaji wa mwinuko wa barabara
- Usanifu wa ramani kwa kompyuta
UCHORAJI RAMANI KUTOKANA NA PICHA ZA
ANGA
- Kuchapa ramani kutoka kwenye kompyuta katika rangi moja au nyingi
4. Teknolojia ya
Kisasa
Kwa kutumia teknolojia ya kisasa,
idara ina uwezo wa kuchora na kutoa ramani katika mfumo wa kompyuta. Ramani za
baadhi ya maeneo hususan ya kati ya Jiji na Manispaa zote nchini ziko katika
mfumo wa kompyuta. Ramani au Kumbukumbu Kuu ya Uoto wa Tanzania ipo katika
mfumo wa kompyuta
5. Upatikanaji wa
Bidhaa na Huduma za Idara.
5.1 Huduma za Upimaji na
Ramani
Bidhaa za kawaida zikiwemo ramani,
picha za anga huuzwa katika duka la ramani lililopo jengo la Casino katika
makutano ya barabara za Kivukoni Front na Luthuli, jijini Dar es Salaam
5.2 Bidhaa na huduma ya pekee
hupatikana kwa maombi ya mteja.
Kwa maelezo zaidi,
wasiliana na:
Mkurugenzi,
Idara
No comments:
Post a Comment