HUDUMA ZA MAEMDELEO YA ARDHI
Uthamini
1. Uthamini ni
nini?
Uthamini ni utaratibu na utaalam wa
kukadiria na kushauri kuhusu thamani ya mati inayohamishika (kama vile samani,
mashine, na magari): na isiyohamishika (kama vile ardhi, majengo na mazao)
Hivyo neno uthamini linatokana na neno thamani.
2. Thamani ni
nini?
Thamani kwa ujumla wake inaweza
kuelezewa kama bei inayolipwa kwa ajili ya
kupata kitu. Lakini kwa lugha ya
kitaaluma: thamani hususan ya mali isiyohamishika kwa mfano
ardhi inahusisha;-
- Upatikanaji wake (availability)
- Ubora na matumizi yake (utility)
- Mahali ilipo (location)
- Umiliki wake (ownership.
3. Je, Ardhi ina
thamani?
Ndiyo kwa sababu:
- Ardhi ni rasilimali ya msingi ambayo shughuli zote za
kijamii, kiuchumi na kimaendeleo zinafanyika juu yake. Kwa Tanzania,
asilimia takribani,themanini (80%) ya Wananchi wa vijiji hutegemea ardhi
kwa maisha yao ya kila siku kwa chakula, kipato na mahitaji mengine.
- Ardhi ni rasilimali adimu ambayo hushindaniwa na watu
au shughuli mbalimbali na hivyo kuifanya iwe na thamani kubwa.
- Ardhi humilikiwa kiserikali na kimila kwa sheria,
kanuni na taratibu zinazokubalika. Ni kutokana na thamani ya ardhi, watu
hulazimika kujisikia kumiliki ardhi na kuishindania.
Nini umuhimu wa Uthamini?
Kuongezeka kwa ushindani wa mahitaji
ya ardhi inayomilikwa kiserikali kulinganisha na ardhi iliyopo kumejenga
umuhimu wa kusimamia na kutawala ardhi hiyo adimu kwa umakini mkubwa.
Hivyo ni nguzo mojawapo ya
utawala na usimamizi bora wa ardhi kwa kuwezesha
maamuzi ya maendeleo bora ya ardhi kufanyika.
5. Mini sababu za
Uthamini?
Uthamini unaweza kutakiwa kwa
madhuni mbalimbali kama vile:-
- Ushauri wa maamuzi ya uuzaji na ununuzi.
- Kupangisha/kushauri bei ya pango.
- Rehani/mikopo
- Bima
- Ukadiriaji wa misingi ya utozaji kodi, ushuru na ada
mbalimbali za kiserikali na uchumi.
- Sababu za kiuhasibu na mizani. •«* Ukadiriaji fidia
kutokana na utwaaji ardhi.
6.
Uthamini kwa madhumuni ya Fidia:
Dhana ya fidia:
Kwa kuwa Ardhi ya Tanzania ni mali
ya wananchi wote, Rais ndiye mwenye dhamana ya kuilinda kwa manufaa ya wote.
Hata hivyo mwananchi anaruhusiwa kuitumia na pale ambapo inahitajika kutwaliwa
kwa ajili ya sababu nyingine hasa za maendeleo ya taifa, basi mmiliki wa ardhi
hiyo anastahili kulipwa fidia.
7. Nini Misingi ya
uthamini wa fidia?
- Uthamini na ulipwaji wa fidia hufanyika kulingana na
misingi ya taaluma na kwa kuzingatia sheria ya Ardhi Na. 4 ya 1999
(kifunguNa3 (I) (g) na kanuni zake husika)
- Misingi ya uthamini wa fidia inatawaliwa na agizo la
sheria ya uthamini wa haki, kamilifu na kulipwa kwa wakati muafaka (fair,
full and prompt compensation)
Kulingana na kifungucha 3 cha sheria
ya Ardhi Na.4 ya 1999 na kanuni (Taarifa ya Serikali Na.78 ya 2001) za fidia
inapaswa ijumuishe yafuatayo pale panapohusika:-
- Thamani ya ardhi na mali isiyohamishika (unexhausted
improvements)
- Posho ya usumbufu (disturbance allowance)
- Posho ya usafiri (transport allowance)
- Posho ya upotevu wa makazi(loss of accommodation)
- Posho ya upotevu wa faida(loss of profit)
- Gharama za awali za kupata ardhi.
- Kama fidia imecheleweshwa ilipwe pamoja na riba kwa
kiwango cha soko huria.
- Mwenye shamba kuonyesha mipaka ya shamba au mali yake
- Kuchukua taarifa ya ukubwa
8. Taratibu za
Uthamini wa Fidia
Uthamini hutekelezwa katika hatua
kuu nne:
(a) Maandalizi ya awali (Pre-
site Inspection):
- Mthamini anatembelea eneo husika, ili kubaini ukubwa wa
kazi na wahusika.
- Maandalizi ya vitendea kazi na viwango vya thamani.
(b) Ukaguzi wa mali
- Kumtambua mwenye mali ya kumworodhesha katika fomu ya
ukaguzi.
- Kutoa namba ya kumbukumbu wa eneo husika kwa kutumia
GPS au ramani ya picha za anga
- Kuhesabu mazao ili kubaini idadi na kiwango cha ukuaji
wa mazao ya aina mbalimbali
- Kukagua majengo na kuchukua taarifa zote husika ikiwa
ni pamoja na vipimo.
- Kujaza taarifa ya majengo au idadi ya mazao kwenye fomu
ya ukaguzi
- Kumpiga picha mfidiwa mbele ya mali yake akiwa ameshika
bango lenye namba ya kumbukumbu iliyotolewa.
- Kuhakikisha fomu ya ukaguzi imesainiwa na mwenye mali.
- Mthamini husika na kiongozi wa serikali ya Mtaa
ambaye atathibitisha uhalali wa mfidiwa.
c) Ukokotoaji wa
thamani:
- Kuhamisha taarifa toka fomu ya ukaguzi na kuingiza
kwenye fomu ya ukokotoaji thamani.
- Kukokotoa mahesabu ya thamani kwa kutumia viwango
vilivyotolewa na Ofisi ya Mthamini Mkuu ili kupata thamani ya mali husika
- Kuwasilisha fomu zote kwa Mthamini Mkuu kwa ajili ya
kuthibitishwa.
(d) Utayarishaji wa Hati za Fidia (compesantion
Schedules)
Baada ya kumaliza udhamini na
kuandaa taarifa; majedwali ya fidia yanatayarishwa yakionyesha:
- Majina ya walipwaji
- Mali zitakazolipwa fidia
- Thamani ya fidia kwa kila mali
Kisha jumla ya fidia itasainiwa na:
- Mthamini Mkuu
- fisa Ardhi anayeshughulika na zoezi hilo.
- Katibu Kata wa Kata husika
- Mkuu waWilaya husika
- Mkuu wa Mkoa.
(e) Ulipaji wa Fidia
Husimamiwa na Katibu Mtendaji kwa
kuwatambulisha walipwaji fidia
9. Taratibu za Uthamini
kwa Ujumla;
Kwa mwananchi anayehitaji huduma ya
uthamini kwa ujumla kuna taratibu za utendaji zinazohusisha:-
- Maombi ya uthamini kwa maandishi yakiambatanishwa na kivuli
cha hati au barua ya toleo.
- Ili kumwezesha Mthamini aifanye kazi yake kwa ufanisi
mkubwa , ushirikiano kati ya mteja na mthamini unaitajika sana. Mteja
anapaswa kuwa mwaminifu kwa kujibu maswali mbalimbali atakayoulizwa na
Mthamini
- Mthamini hutakiwa kufanya ukaguzi wa mali (Physical
Site Inspection)
- Kisha ukokotoaji wa thamani hufanyika kwa kuzingatia
viwango na kanuni za kitaalamu na za kisheria na hatimaye taarifa ya
uthamini huandaliwa.
- Mteja hutakiwa kulipia ada ya udhamini kabla ya taarifa
ya uthamini kuthibitishwa.
- Mwisho taarifa ya uthamini huthibitishwa na Mthamini
Mkuu na kisha kukabidhiwa kwa mwombaji.
Kwa maoni au maswali wasiliana na:
Kitengo cha Uthamini
idara ya Ardhi
S.LP.9230
DAR ES Salaam,
Email:-agcv@ardhi.go.tz
KUMILIKISHA ARDHI
1. Aina za ardhi
Kulingana na sheria ya ardhi Na. 5
ya mwaka 1999, ardhi ya Tanzania ipo katika makundi matatu:-
- Ardhi ya Kijiji, (Village Land)
- Ardhi ya Hifadhi (Reserved,Land) na
- Ardhi ya Jumla (General Land).
2. Aina za miliki
za ardhi
Kuna aina mbili za miliki ya ardhi
zinazotambulika kisheria:
- Miliki ya kupewa na Serikali (Granted Right of
Occupancy)
- Miliki ya Kimila (Deemed Right of Occupancy)
3. Makundi ya Ardhi ya
Jumla
- Ardhi iliyopimwa
- Ardhi isiyopimwa Ardhi iliyopimwa ndiyo pekee inayoweza
kutolewa na Kamishna wa Ardhi
Maombi ya Ardhi
Ardhi
hutolewa na kamati za
kugawa ardhi
kwenye ngazi mbalimbali kufuatia:-
- Maombi kwa kujaza fomu maalum
- Maelekezo ya Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya Ardhi
4. Madarakaya
Waziri wa Ardhi
Mheshimiwa
Waziri wa Ardhi anaweza
kuelekeza kuwa ardhi fulani itolewe kwa mnada au
zabuni. Kama akielekeza hivyo, kamati itatoa tangazo lenye nia hiyo kwa muda wa
siku 21.Tangazo hilo litaonyesha nambari za viwanja vilivyokusudiwa na mahali
vilipo.
Kamati za kugawa ardhi
6. Aina ya maombi
yanavyo-shughulikiwa katika kila
ngazi
6. 1 Ngazi ya Halmashauri za Wilaya,
Miji, Manispaa au Jiji
Kamati itatoa viwanja ndani ya
mipaka ya Wilaya vya aina zifuatazo:-
- Ujenzi wa ofisi za Serikali.
- Makazi, biashara na viwanja vya huduma
- Hoteli na viwanda
- Ibada na huduma za jamii na
- Mashamba yasiyozidi ekari 500 vinginevyo kwa kibali cha
Mheshimiwa Waziri wa Ardhi.
6.2 Ngazi yaWizara:
- Uanzishaji wa Miji mipya
- Viwanja vya Mashirika au taasisi za Kigeni
- Viwanja vya ufukweni na visiwa vidogo.
- Viwanja vya ujenzi wa makazi ya pamoja (housing
estates) vyenye maeneo yanayozidi hekta tano (5ha.)
- Ardhi inayotolewa kwaTIC kwa ajili ya
uwekezaji.
- Ardhi kwa matumizi yenye maslahi ya kitaifa.
- Mashamba yanayozidi ekari 500
7. Utaratibu wa kumilikishwa ardhi
Baada ya kamati kukamilisha zoezi
la kugawa ardhi, mambo yafuatayo
yatafanyika:-
- Kamati itatoa tangazo
- Waombaji waliopewa ardhi/watapewa barua za toleo
(letters of offer)
- Waliopewa ardhi watalipia adana kodi zilizoainishwa
na kurejesha stakabadhi za malipo.
8. Utayalishaji wa Hati
- Kutayarisha ramani ndogo (deed plans) na kuchapa rasimu
ya hati kwenye ofisi ilipotolewa barua ya toleo.
- Mmiliki kusaini hati mbele ya shahidi anayekubalika
kisheria kama Hakimu,Wakili,Afisa Ardhi, nk.
- Hati kusainiwa na Kamishna wa Ardhi
- Hati kusajiliwa na Msajili Hati katika kanda husika
(Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Moshi na Mbeya) kutegemea kiwanja
kipo kanda ipi.
Miliki ya Uhamisho
Miliki ya ardhi inaweza kupatikana
kwa uhamisho wakati ambapo mtu anayeomba kuhamishiwa miliki hiyo anao
uthibitisho kuwa:-
- amenunua maendelezo juu ya ardhi hiyo,
- amepewa zawadi ya maendelezo juu ya ardhi
- amerithi maendelezo husika
Katika utaratibu huu mwananchi
huomba kibali cha kuhamisha miliki yake. Maombi hayo
huambatanishwa na:-
- Ushahidi au uthibitisho wa ununuzi, kupewa zawadi au
urithi.
- Taarifa ya uthamini iliyothibitishwa na Mthamini Mkuu
wa Serikali. »
- Stakabadhi ya kodi ya ardhi ya mwaka husika
- Fomu ya taarifa ya kusudio la uhamisho
- Fomu ya maombi ya idhini ya uhamisho
- Picha za utambulisho (za pande zote zinazohusika)
- Nakala mbili za hati ya uhamisho
- Hati ya kumiliki ardhi au barua ya toleo na ushuhuda wa
malipo pale ambapo hati haijatolewa.
Aidha Kamishna anaweza kukataa kutoa
kibali iwapo hakuridhika. Kibali kikitolewa, kama miliki husika ilikuwa
inamilikiwa kwa hati, uhamisho huo utasajiliwa na Msajili wa Hati. Kama hati
ilikuwa haijatayarishwa, hati itatayarishwa kwa jina la mmiliki mpya.
Kwa maoni au maswali wasiliana na:
Kamishna wa Ardhi
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya
Makazi,
S.L.P. 9230
Dar es Salaam,
Simu:2ll8303,