Pamoja na ulinzi wa hali ya juu
ardhini, ndege za kivita zitatawala anga ya Tanzania kwa saa 24 kwa siku zote
atakazokaa.
Dar es Salaam. Idara ya
Ujasusi ya Marekani imeweka bayana kwamba inajitegemea kwa ulinzi katika ziara
nzima ya Rais Barack Obama kwa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini
na Senegal.
Kwa mujibu wa taarifa ya
idara hiyo, katika kuhakikisha usalama wa kutosha wakati wa ziara ya Obama
tayari maofisa wao wameshakamilisha maandalizi ya kiusalama katika nchi zote
anazotarajiwa kutembelea.
Meli ya kivita kutua
bandarini
Katika kuchukua hatua
hizo, meli kubwa kabisa ya kivita yenye hospitali maalum zipo tayari kwa ya
kambi maalumu katika bandari maalum za nchi atakazotembelea, kwa ajili ya
kukabiliana na dharura yoyote ya kiafya ya Obama na familia yake.
Ili kuwawezesha maofisa
wa kijasusi wa Marekani, ndege ya kijeshi ndiyo itakayobeba magari 56 zikiwemo
limousine 14 na magari matatu maalumu ya kubeba mizigo.
Malori hayo yatakuwa
yakibeba vioo ambavyo ni vizuizi maalumu vya risasi na milipuko kwa ajili ya
kuongeza ulinzi kwenye hoteli atakazolala yeye na familia yake.
Ndege za kivita kutawala
anga
Ndege za kivita zitakuwa
zikiruka kwa zamu wakati wote muda wa sasa 24 kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi
katika sehemu atakayokuwa Rais Obama na kudhibiti anga yote kwa wakati huo
dhidi ya ndege yoyote ngeni itakatosogea usawa wao.
Kwa mujibu wa uchunguzi
uliofanywa na Mwananchi, hakuna Maandalizi ya safari hiyo ambayo tayari
yamekamilika yanapolinganishwa na safari nyingine za aina hiyo zilizowahi
kufanyika, waraka maalumu kuhusu suala la usalama unaonesha kwamba kumekuwa na
juhudi za ziada zakuhakikisha ulinzi wa Amiri jeshi huyo Mkuu wa Marekani akiwa
nje ya nchi.
Kabla ya safari yake kwa
nchi za Afrika, Obama atatembelea Ireland na Ujerumani ikiwa ni sehemu ya
kuongeza changamoto inayokabili masuala ya usalama wake.
Lakini zaidi, safari ya
Obama kwa nchi za Afrika inadhaniwa kuwa inayolazimisha waandaaji kuwa na
umakini wa hali ya juu na kuifanya iwe aghali zaidi katika utawala wa Obama
kuliko ziara katika nchi za ulaya, kwa mujibu wa wataalamu wa mipango.
Familia ya rais huyo inatarajiwa kutembelea nchi
tatu za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senagal kuanzia Juni 26 hadi
Julai 3 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment