Wednesday, May 15, 2013

ILI NDOTO YAKO ITIMIE



 “HUU NDIO UJASIRIAMALI”
USISHINDWE KUANZISHA BIASHARA KWA KUKOSA MAARIFA!
“ili ndoto  yako itimie”



Tamko la mwelekeo
Benki ya Azania inakusudia kuwa benki inayoongoza katika kutoa huduma za kibenki
kwa wateja wadogo  na wa kati.


Hatua  muhimu  za kuzingatia!


1. Nyambulisha na uainishe mradi  unaotaka kufanya  kwa msingi  wa wazo  linalotekelezeka

2. Fursa  ya biashara hutokana na yafuatayo
a. Tathmini ya wazo lako la biashara.
b. Tathmini ya kina ya mahitaji ya soko ambalo biashara yako italenga.
c. Tathmini ya kina ya bidhaa zako na huduma zako.
d. Tathmini ya kina na jinsi bidhaa yako/huduma yako itakavyokidhi mahitaji ya soko ulilolenga
e. Fikiria na ufafanue walengwa/watumiaji wa bidhaa au huduma zako.
f.  Tathimini taratibu za kisheria na kiutawala kuhusu biashara unayotaka kuanzisha.

3. Angalia ushindani uliopo  sokoni (husisha yafuatayo)
a. Angalia na uorodheshe  biashara nyingine zinazotoa huduma/bidhaa kama unazotaka kutoa wewe.
b. Angalia na ujiulize kama wapo washindani wengine wapya wanaotaka kuingia kwenye
biashara hiyo hiyo unayokusudia.

c. Jiulize changamoto  zilizopo na vikwazo vilivyopo (kisheria, kimtaji, au vinginevyo) vinavyoweza kuzuia biashara nyingine zinazofanana na biashara yako kuanzishwa.
d. Jiulize na uorodheshe  upekee  wa bidhaa/huduma zako (jiulize sababu za kumfanya mtu ahitaji bidhaa/huduma yako badala ya  bidhaa/huduma nyingine zilizopo sokoni)

4. Angalia uwezekano wa biashara yako kuendelea na kukua  (ujibu yafuatayo)

a. Utawafikiaje walengwa wa biashara yako (Ni
kwa vipi walengwa wako watajua kuhusu bidhaa na huduma zako)?
b. Utasambazaje/ fikishaje bidhaa/huduma zako (Bidhaa zako zitafikaje kwa wauzaji wa rejareja au huduma zako zitafikaje kwenye maeneo uliyokusudia na maeneo  hayo ni yapi)?
c. Nini makadirio yako ya wafanyakazi unaohitaji kwa miaka miwili ya kazi (wafanyakazi wangapi utahitaji mwaka wa kwanza, na wangapi utahitaji mwaka wa pili)?
d. Unahitaji ufanye nini ili biashara yako ipate faida na itachukua muda gani kuwa na faida?
e. Nini matarajio yako ya mapato na matumizi kwa miaka 4 ya kazi (ni mapato na matumizi kiasi gani katika mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, wa tatu na wa nne)?

f.  Unahitaji mtaji wa kiasi gani (kiasi gani cha fedha unachohitaji kuwekeza) katika mwaka wa kwanza,wa pili, wa tatu na wa nne ili kuendesha biashara yako?
g. Utawezaje kupata kiasi hicho cha mtaji? Je ni kwa kuanza kuweka akiba katika benki au kuomba mkopo na kwa gharama gani?. Je mchango wako katika mtaji ni kiasi gani?
h. Je mradi wako unaweza ukabeba gharama zinazotakiwa kiundeshaji na bado ukazalisha faida?

5. Uzoefu  wako  katika  ujasiriamali na uwajibikaji.

a. Tathmini kiwango chako cha elimu na uzoefu wako unaohusiana  na wazo lako la biashara na mahusiano uliyo nayo na wadau muhimu ki- sekta wewe kama mjasiriamali.
b. Tathmini kuhusu wataalam wa fani mbalimbali ambao utahitaji kuwatumia katika maeneo ambayo wewe si mtaalam wala mzoefu ili kufanikisha uanzishaji na uendeshaji wa biashara yako.
c. Kwa ufupi tathmini nia/malengo yako ya kutimiliza kuanza na kukua kwa biashara ukizingatia muda utakaotumia kupanga, muda unaokusudia kutumia katika mradi, kiwango cha fedha za kwako mwenyewe unachoridhia kuweka katika mradi n.k.

Z I N G A T I A  H A Y A  A N D A A  T U O N E


ili  ndoto  yako  ya  kumiliki  na  kuendesha  biashara  endelevu  itimie


Azania Bank Limited Masdo House Samora Avenue
Box 9271Dar es Salaam, Tanzania
Tel: 255 22 2118014, 2117998 - 9, 2118025 - 6
Fax 255 22 2118010 - 1 www.azaniabank.co.tz

 

No comments:

Post a Comment