Monday, September 19, 2016

Rais Magufuli Apokea Taarifa Ya Tetemeko La Ardhi Mkoani Kagera, Akabidhiwa Msaada Wa Dola Laki Mbili Kutoka Kwa Rais Museveni Wa Uganda

Jumamosi, SEPTEMBER 17, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na

Thursday, January 1, 2015

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MH: DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, DISEMBA 22, 2014.


Rais Kikwete akisoma hotuba yake kwa Wazee wa mkoa wa Dar Es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar Es Salaam.

Shukrani

Mheshimiwa Makamu wa Rais;
Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM;
Mkuu wa Mkoa wa

MAONI BAADA YA HOTUBA YA RAIS YA DISEMBA 22,2014


Sehemu ya wazee wa Mkoa Dar es Salaam wakishangilia kuunga mkono kufukuzwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maenedeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana. Picha na Venance Nestory .




Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow imepokewa kwa

Wednesday, January 8, 2014

RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE KWA CHADEMA

*Nyaraka hii imechomolewa kwa siri toka Chadema makao makuu

RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE KWA CHADEMA

UCHUNGUZI WA MWENENDO WA KISIASA WA ZITTO Z. KABWE NDANI NA NJE YA CHADEMA.


UTANGULIZI:
Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa anakisaliti chama.
Hilo liliilazimu timu ya kijasusi ya chama kuanza kufuatilia nyendo zake kwa ukaribu zaidi usiku na mchana ili kujiridhisha pasipo kuacha chembe ya mashaka. Ifahamike kuwa chama kina idara ya ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake yenye uwezo wa kufuatilia nyendo za majasusi wa nje na viongozi na wanachama wake popote walipo kwa masaa 24. Baada ya kujiridhisha kuwa mwenendo wake ni wa mashaka, bila kusita timu ya ujasusi ilianza kazi rasmi ya ujasusi dhidi ya nyendo zote za Zitto Zuberi Kabwe


MAMBO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI DHIDI YA ZITTO KABWE.

Kumfuatilia yeye binafsi nyendo zake.
Kufuatilia mawasiliano yake ya simu.
Kufuatilia mawasiliano yake ya barua pepe.
Kufuatilia pato lake nje ya kazi zake halali za kibunge.

SEHEMU YA KWANZA 2008

Chombo chetu cha ujasusi tulichokipandikiza kwa siri katika nyendo zote za Zitto Kabwe na ndani ya vikao vya mwanzo kabisa vya Zitto na viongozi serikalini, nahata vile vikao muhimu vya idara ya ujasusi ya chama cha mapinduzi (ccm), kinatupa fursa ya kuweka msingi wa kuimarisha chama cha CHADEMA na kutenda haki kidemokrasia kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla:

Mnamo Jumatatu ya tarehe 16/6/2008 saa 09:46 asubuhi, Mh Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba +255754787550 alipokea simu kutoka kwa Ramadhani Ighondu mwenye namba +255717760473 ambaye ni afisa Usalama wa Taifa anayefanya kazi ikulu hivi sasa. Alijitambulisha kuwa yeye ni Usalama wa Taifa ametumwa na mkuu wake wa kazi aje aongee na Zitto, Maelezo ya msingi katika simu hii ilikuwa ni bwana Ramadhani Ighondu kuomba miadi ya kuonana kutokana na agizo la mkuu wake wa kazi.

Siku sita baadae yaani Jumatatu ya tarehe 23/6/2008 saa 07:52 asubuhi, Zitto alipigiwa tena simu na Ramadhani Ighondu akimkumbusha maongezi yao waliyo fanya siku 6 zilizopita na kumuomba siku hiyo jioni waonane, ingawa Zitto alionekana kusita kidogo lakini baadae alikubali, Walikubaliana wakutane Sea Cliff Hotel, ilipofika jioni ya siku hiyo Zitto akiwa na marafiki zake wawili Omar Lyasa na Abdalah Said walifika Sea Cliff Hotel wakaketi na kuagiza vinywaji, Baada ya kama dakika kumi hivi Zitto alipokea simu ikimuelekeza alipo bwana Ramadhani Ighondu kisha Zitto akawaambia marafiki zake wamsubiri kidogo, akaondoka kuelekea aliko elekezwa…..

Mashariki mwa lango kuu la kuingilia Sea Cliff Hotel mita kama tatu tu kuna mlango mdogo unaoelekea kwenye vyumba maalumu (VIP), chumba namba 8 ndicho Zitto alichokuwa anaelekezwa kwa simu kuingia, chumba hiki kina meza moja na sofa zilizo zunguka meza ile zenye uwezo wakukaliwa na watu watano hadi sita, Ndani ya chumba kile Zitto anakutana na watu watatu ambao ni Steven Wasira, Ramadhani Ighondu na Abdalla Punja (hawa wote ni TISS)

Saturday, June 15, 2013

Ndege maalumu za kivita kutawala anga Dar

Pamoja na ulinzi wa hali ya juu ardhini, ndege za kivita zitatawala anga ya Tanzania kwa saa 24 kwa siku zote atakazokaa.


Dar es Salaam. Idara ya Ujasusi ya Marekani imeweka bayana kwamba inajitegemea kwa ulinzi katika ziara nzima ya Rais Barack Obama kwa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senegal.