Saturday, May 18, 2013

FISI aitwae "MASIKA



                          
                                   Hadithi Ya Fisi Mvivu aitwaye Masika

Hadithi Hadithi,
Hadithi njoo, uwongo njoo, utamu kolea.
Hapo  zamani  za  kale  palikuwa  na  Fisi  aitwaye  Masika.  Masika  alikuwa  ni  Fisi  mvivu  sana  asiyependa
kufanya kazi ya aina yoyote, alipenda tu kulala muda wote. Tangia enzi zake alivyokuwa anasoma shule,
hakupenda  kukaa  darasani  na  kumsikiliza  mwalimu.  Aliwaza  tu  kurudi  nyumbani  na  kulala  kitandani
kwake.  Masika  alikuwa  ni  mvivu  kiasi  kwamba  mara  nyingine  mwalimu  wake  akifundisha  darasani,
Masika  alikuwa  akisinzia.  Mwalimu  akimuuliza  kwanini  anafanya  hivyo  alilia  kwa  sauti  ya  unyonge!
“Uuuwiii, uuuwiii, nimechoka, uuuuuwiii.” Afikapo tu nyumbani alijivuta mpaka kitandani na kulala huku
akikoroma. Wazazi wake walikuwa wakimtuma kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia lakini Masika hakuweza
kufanya hivyo kwa ajili ya uvivu wake, Masika alipenda sana kucheza tu na baadae akichoka analala bila
hata ya kuoga.

Thursday, May 16, 2013

Baadhi yaNjia Unazoweza Kutumia Kupata wazo Bora kabisa la Biashara


Wazo laBiashara ni moja ya mambo yanayowaumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ilikuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii  nzima,

HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA

1. TUMIA UJUZI ULIONAO
Ujuzi  ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupatawazo la Biashara, Mfano kama wewe umeajiliwa nani mtaalamu wa ramani, kwanini usianzishe na wewe kitengo cha biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni kuchapisha vitabu kwanini usianzishe kiwanda kidogo cha kuchapisha vitabu cha kwako?
Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza naya kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasiliamali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazofanya nakwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe.


Huduma za Upimaji Ramani



Majukumu ya Idara kwa Ujumla

Majukumu ya Idara

Upimaji na Ramani ni Idara katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi. Jukumu lake kubwa ni usimamizi wa upimaji ardhi na utayarishaji wa ramani na plani mbalimbali za nchi mijini na vijijini. Ramani hizo ni msingi wa kubuni, kutekeleza na kuratibu mipango ya maendeleo juu ya ardhi katika sekta na kwa matumizi mbalimbali kama:

  • Umilikishaji ardhi
  • Kupanga matumizi ya ardhi
  • Utalii
  • Mawasiliano
  • Makazi
  • Kilimo
  • Hifadhi ya mazingira
  • Utafiti na uchimbaji madini

JE, WEWE NI MMOJA WA VIJANA WENYE TATIZO LA KUJICHUA AU UNAMFAHAMU MWENZAKO MWENYE TABIA HIYO? SOMA HAPA UJIELIMSHE


Stop masturbation 
you will die barren 

Kujichua ni tabia ya kingono ambayo inapofanywa kwa kiwango kikubwa inaleta matatizo ya kiumbo na kisaikolojia kwa anayefanya tendo hilo.
Na katika kipindi cha zama hizi ambazo majarida, vipindi na hata mitandao mingi inaonyesha picha za ngono ndio kunaifanya tabia hii kushamiri kwa kiwango kikubwa.
Kwani vijana wengi wanaingia katika mchezo huu wa kujiridhisha wenyewe bila kujua madhara yatakayokuja baadaye.


Huduma za Maendeleo ya Ardhi



HUDUMA ZA MAEMDELEO YA ARDHI

Uthamini

1.    Uthamini ni nini?

Uthamini ni utaratibu na utaalam wa kukadiria na kushauri kuhusu thamani ya mati inayohamishika (kama vile samani, mashine, na magari): na isiyohamishika (kama vile ardhi, majengo na mazao) Hivyo neno uthamini linatokana na neno thamani.

2.    Thamani ni nini?

Thamani kwa ujumla wake inaweza kuelezewa   kama   bei   inayolipwa kwa ajili ya kupata kitu. Lakini kwa lugha    ya     kitaaluma:    thamani hususan ya mali isiyohamishika kwa mfano ardhi inahusisha;-   

  • Upatikanaji wake (availability)
  • Ubora na matumizi yake (utility)
  • Mahali ilipo (location)
  • Umiliki wake (ownership.

3.    Je, Ardhi ina thamani?

Ndiyo kwa sababu:

  • Ardhi ni rasilimali ya msingi ambayo shughuli zote za kijamii, kiuchumi na kimaendeleo zinafanyika juu yake. Kwa Tanzania, asilimia takribani,themanini (80%) ya Wananchi wa vijiji hutegemea ardhi kwa maisha yao ya kila siku kwa chakula, kipato na mahitaji mengine.




  • Ardhi ni rasilimali adimu ambayo hushindaniwa na watu au shughuli mbalimbali na hivyo kuifanya iwe na thamani kubwa.
  • Ardhi humilikiwa kiserikali na kimila kwa sheria, kanuni na taratibu zinazokubalika. Ni kutokana na thamani ya ardhi, watu hulazimika kujisikia kumiliki ardhi na kuishindania.

Nini umuhimu wa Uthamini?

Kuongezeka kwa ushindani wa mahitaji ya ardhi inayomilikwa kiserikali kulinganisha na ardhi iliyopo kumejenga umuhimu wa kusimamia na kutawala ardhi hiyo adimu kwa umakini mkubwa. Hivyo   ni   nguzo   mojawapo   ya utawala na usimamizi bora wa ardhi kwa    kuwezesha    maamuzi    ya maendeleo bora ya ardhi kufanyika.

5.    Mini sababu za Uthamini?

Uthamini unaweza kutakiwa kwa madhuni mbalimbali kama vile:-  

  • Ushauri wa maamuzi ya uuzaji na ununuzi.
  • Kupangisha/kushauri bei ya pango.
  • Rehani/mikopo
  • Bima
  • Ukadiriaji wa misingi ya utozaji kodi, ushuru na ada mbalimbali za kiserikali na uchumi.
  • Sababu za kiuhasibu na mizani. •«* Ukadiriaji fidia kutokana na utwaaji ardhi.

6.    Uthamini kwa madhumuni ya Fidia:

Dhana ya fidia:

Kwa kuwa Ardhi ya Tanzania ni mali ya wananchi wote, Rais ndiye mwenye dhamana ya kuilinda kwa manufaa ya wote. Hata hivyo mwananchi anaruhusiwa kuitumia na pale ambapo inahitajika kutwaliwa kwa ajili ya sababu nyingine hasa za maendeleo ya taifa, basi mmiliki wa ardhi hiyo anastahili kulipwa fidia.

7.    Nini Misingi ya uthamini wa fidia?

  • Uthamini na ulipwaji wa fidia hufanyika kulingana na misingi ya taaluma na kwa kuzingatia sheria ya Ardhi Na. 4 ya 1999 (kifunguNa3 (I) (g) na kanuni zake husika)
  • Misingi ya uthamini wa fidia inatawaliwa na agizo la sheria ya uthamini wa haki, kamilifu na kulipwa kwa wakati muafaka (fair, full and prompt compensation)

Kulingana na kifungucha 3 cha sheria ya Ardhi Na.4 ya 1999 na kanuni (Taarifa ya Serikali Na.78 ya 2001) za fidia inapaswa ijumuishe yafuatayo pale panapohusika:-

  • Thamani ya ardhi na mali isiyohamishika (unexhausted improvements)
  • Posho ya usumbufu (disturbance allowance) 
  • Posho ya usafiri (transport allowance)
  • Posho ya upotevu wa makazi(loss of accommodation)
  • Posho ya upotevu wa faida(loss of profit)
  • Gharama za awali za kupata ardhi.
  • Kama fidia imecheleweshwa ilipwe pamoja na riba kwa kiwango cha soko huria.
  • Mwenye shamba kuonyesha mipaka ya shamba au mali yake
  • Kuchukua taarifa ya ukubwa

8.   Taratibu za Uthamini wa Fidia

Uthamini hutekelezwa katika hatua kuu nne:

(a) Maandalizi ya awali (Pre-
site Inspection):

  • Mthamini anatembelea eneo husika, ili kubaini ukubwa wa kazi na wahusika.
  • Maandalizi ya vitendea kazi na viwango vya thamani.

(b) Ukaguzi wa mali

  • Kumtambua mwenye mali ya kumworodhesha katika fomu ya ukaguzi.
  • Kutoa namba ya kumbukumbu wa eneo husika kwa kutumia GPS au ramani ya picha za anga
  • Kuhesabu mazao ili kubaini idadi na kiwango cha ukuaji wa mazao ya aina mbalimbali
  • Kukagua majengo na kuchukua taarifa zote husika ikiwa ni pamoja na vipimo.
  • Kujaza taarifa ya majengo au idadi ya mazao kwenye fomu ya ukaguzi
  • Kumpiga picha mfidiwa mbele ya mali yake akiwa ameshika bango lenye namba ya kumbukumbu iliyotolewa.
  • Kuhakikisha fomu ya ukaguzi imesainiwa na mwenye mali.
  • Mthamini husika na kiongozi wa serikali ya Mtaa ambaye atathibitisha uhalali wa mfidiwa.

c)    Ukokotoaji wa thamani:

  • Kuhamisha taarifa toka fomu ya ukaguzi na kuingiza kwenye fomu ya ukokotoaji thamani.
  • Kukokotoa mahesabu ya thamani kwa kutumia viwango vilivyotolewa na Ofisi ya Mthamini Mkuu ili kupata thamani ya mali husika
  • Kuwasilisha fomu zote kwa Mthamini Mkuu kwa ajili ya kuthibitishwa.

(d) Utayarishaji wa Hati za Fidia (compesantion Schedules)

Baada ya kumaliza udhamini na kuandaa taarifa; majedwali ya fidia yanatayarishwa yakionyesha:

  • Majina ya walipwaji
  • Mali zitakazolipwa fidia
  • Thamani ya fidia kwa kila mali

Kisha jumla ya fidia itasainiwa na:

  • Mthamini Mkuu
  • fisa Ardhi anayeshughulika na zoezi hilo.
  • Katibu Kata wa Kata husika
  • Mkuu waWilaya husika
  • Mkuu wa Mkoa.

(e) Ulipaji wa Fidia

Husimamiwa na Katibu Mtendaji kwa kuwatambulisha walipwaji fidia

9.   Taratibu za Uthamini kwa Ujumla;

Kwa mwananchi anayehitaji huduma ya uthamini kwa ujumla kuna taratibu za utendaji zinazohusisha:-

  • Maombi ya uthamini kwa maandishi yakiambatanishwa na kivuli cha hati au barua ya toleo.
  • Ili kumwezesha Mthamini aifanye kazi yake kwa ufanisi mkubwa , ushirikiano kati ya mteja na mthamini unaitajika sana. Mteja anapaswa kuwa mwaminifu kwa kujibu maswali mbalimbali atakayoulizwa na Mthamini
  • Mthamini hutakiwa kufanya ukaguzi wa mali (Physical Site Inspection)
  • Kisha ukokotoaji wa thamani hufanyika kwa kuzingatia viwango na kanuni za kitaalamu na za kisheria na hatimaye taarifa ya uthamini huandaliwa.

  • Mteja hutakiwa kulipia ada ya udhamini kabla ya taarifa ya uthamini kuthibitishwa.
  • Mwisho taarifa ya uthamini huthibitishwa na Mthamini Mkuu na kisha kukabidhiwa kwa mwombaji.

Kwa maoni au maswali wasiliana na:

Kitengo cha Uthamini

idara ya Ardhi

S.LP.9230

DAR ES Salaam,

Email:-agcv@ardhi.go.tz



KUMILIKISHA ARDHI

1.    Aina za ardhi

Kulingana na sheria ya ardhi Na. 5 ya mwaka 1999, ardhi ya Tanzania ipo katika makundi matatu:- 

  • Ardhi ya Kijiji, (Village Land)
  • Ardhi ya Hifadhi (Reserved,Land) na 
  • Ardhi ya Jumla (General Land).

2.    Aina za miliki za ardhi

Kuna aina mbili za miliki ya ardhi zinazotambulika kisheria:

  • Miliki ya kupewa na Serikali (Granted Right of Occupancy)

  • Miliki ya Kimila (Deemed Right of Occupancy)

3.   Makundi ya Ardhi ya Jumla

  • Ardhi iliyopimwa
  • Ardhi isiyopimwa Ardhi iliyopimwa ndiyo pekee inayoweza kutolewa na Kamishna wa Ardhi



Maombi ya Ardhi
Ardhi   hutolewa   na   kamati   za kugawa     ardhi     kwenye     ngazi mbalimbali kufuatia:-

  • Maombi kwa kujaza fomu maalum
  • Maelekezo ya Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya Ardhi

4.    Madarakaya Waziri wa Ardhi

Mheshimiwa   Waziri    wa   Ardhi anaweza   kuelekeza   kuwa   ardhi fulani itolewe kwa mnada au zabuni. Kama akielekeza hivyo, kamati itatoa tangazo lenye nia hiyo kwa muda wa siku 21.Tangazo hilo litaonyesha nambari za viwanja vilivyokusudiwa na mahali vilipo.

Kamati za kugawa ardhi

6.   Aina ya maombi

yanavyo-shughulikiwa katika kila ngazi

6. 1 Ngazi ya Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji

Kamati itatoa viwanja ndani ya mipaka ya Wilaya vya aina zifuatazo:-

  • Ujenzi wa ofisi za Serikali.
  • Makazi, biashara na viwanja vya huduma
  • Hoteli na viwanda
  • Ibada na huduma za jamii na
  • Mashamba yasiyozidi ekari 500 vinginevyo kwa kibali cha Mheshimiwa Waziri wa Ardhi.





6.2 Ngazi yaWizara:

  • Uanzishaji wa Miji mipya
  • Viwanja vya Mashirika au taasisi za Kigeni
  • Viwanja vya ufukweni na visiwa vidogo.
  • Viwanja vya ujenzi wa makazi ya pamoja (housing estates) vyenye maeneo yanayozidi hekta tano (5ha.)
  •   Ardhi inayotolewa kwaTIC kwa ajili ya uwekezaji. 
  • Ardhi kwa matumizi yenye maslahi ya kitaifa.
  • Mashamba yanayozidi ekari 500

7. Utaratibu wa kumilikishwa ardhi

Baada ya kamati kukamilisha zoezi

la kugawa ardhi, mambo yafuatayo

yatafanyika:-

  • Kamati itatoa tangazo
  • Waombaji waliopewa ardhi/watapewa barua za toleo (letters of offer)
  • Waliopewa ardhi watalipia adana kodi zilizoainishwa na kurejesha stakabadhi za malipo.

8. Utayalishaji wa Hati
  • Kutayarisha ramani ndogo (deed plans) na kuchapa rasimu ya hati kwenye ofisi ilipotolewa barua ya toleo.
  • Mmiliki kusaini hati mbele ya shahidi anayekubalika kisheria kama Hakimu,Wakili,Afisa Ardhi, nk.
  • Hati kusainiwa na Kamishna wa Ardhi
  • Hati kusajiliwa na Msajili Hati katika kanda husika (Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Moshi na Mbeya) kutegemea kiwanja kipo kanda ipi.



Miliki ya Uhamisho
Miliki ya ardhi inaweza kupatikana kwa uhamisho wakati ambapo mtu anayeomba kuhamishiwa miliki hiyo anao uthibitisho kuwa:-

  • amenunua maendelezo juu ya ardhi hiyo,
  • amepewa zawadi ya maendelezo juu ya ardhi
  • amerithi maendelezo husika

Katika utaratibu huu mwananchi huomba kibali cha kuhamisha miliki yake. Maombi hayo

huambatanishwa na:-

  • Ushahidi au uthibitisho wa ununuzi, kupewa zawadi au urithi.
  • Taarifa ya uthamini iliyothibitishwa na Mthamini Mkuu wa Serikali. »
  • Stakabadhi ya kodi ya ardhi ya mwaka husika
  • Fomu ya taarifa ya kusudio la uhamisho
  • Fomu ya maombi ya idhini ya uhamisho
  • Picha za utambulisho (za pande zote zinazohusika)
  • Nakala mbili za hati ya uhamisho
  • Hati ya kumiliki ardhi au barua ya toleo na ushuhuda wa malipo pale ambapo hati haijatolewa.

Aidha Kamishna anaweza kukataa kutoa kibali iwapo hakuridhika. Kibali kikitolewa, kama miliki husika ilikuwa inamilikiwa kwa hati, uhamisho huo utasajiliwa na Msajili wa Hati. Kama hati ilikuwa haijatayarishwa, hati itatayarishwa kwa jina la mmiliki mpya.

Kwa maoni au maswali wasiliana na:

Kamishna wa Ardhi

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya

Makazi,

S.L.P. 9230

Dar es Salaam,

Simu:2ll8303,





Wednesday, May 15, 2013

ILI NDOTO YAKO ITIMIE



 “HUU NDIO UJASIRIAMALI”
USISHINDWE KUANZISHA BIASHARA KWA KUKOSA MAARIFA!
“ili ndoto  yako itimie”



Tamko la mwelekeo
Benki ya Azania inakusudia kuwa benki inayoongoza katika kutoa huduma za kibenki
kwa wateja wadogo  na wa kati.


Hatua  muhimu  za kuzingatia!


1. Nyambulisha na uainishe mradi  unaotaka kufanya  kwa msingi  wa wazo  linalotekelezeka

2. Fursa  ya biashara hutokana na yafuatayo
a. Tathmini ya wazo lako la biashara.
b. Tathmini ya kina ya mahitaji ya soko ambalo biashara yako italenga.
c. Tathmini ya kina ya bidhaa zako na huduma zako.
d. Tathmini ya kina na jinsi bidhaa yako/huduma yako itakavyokidhi mahitaji ya soko ulilolenga
e. Fikiria na ufafanue walengwa/watumiaji wa bidhaa au huduma zako.
f.  Tathimini taratibu za kisheria na kiutawala kuhusu biashara unayotaka kuanzisha.

3. Angalia ushindani uliopo  sokoni (husisha yafuatayo)
a. Angalia na uorodheshe  biashara nyingine zinazotoa huduma/bidhaa kama unazotaka kutoa wewe.
b. Angalia na ujiulize kama wapo washindani wengine wapya wanaotaka kuingia kwenye
biashara hiyo hiyo unayokusudia.

c. Jiulize changamoto  zilizopo na vikwazo vilivyopo (kisheria, kimtaji, au vinginevyo) vinavyoweza kuzuia biashara nyingine zinazofanana na biashara yako kuanzishwa.
d. Jiulize na uorodheshe  upekee  wa bidhaa/huduma zako (jiulize sababu za kumfanya mtu ahitaji bidhaa/huduma yako badala ya  bidhaa/huduma nyingine zilizopo sokoni)

4. Angalia uwezekano wa biashara yako kuendelea na kukua  (ujibu yafuatayo)

a. Utawafikiaje walengwa wa biashara yako (Ni
kwa vipi walengwa wako watajua kuhusu bidhaa na huduma zako)?
b. Utasambazaje/ fikishaje bidhaa/huduma zako (Bidhaa zako zitafikaje kwa wauzaji wa rejareja au huduma zako zitafikaje kwenye maeneo uliyokusudia na maeneo  hayo ni yapi)?
c. Nini makadirio yako ya wafanyakazi unaohitaji kwa miaka miwili ya kazi (wafanyakazi wangapi utahitaji mwaka wa kwanza, na wangapi utahitaji mwaka wa pili)?
d. Unahitaji ufanye nini ili biashara yako ipate faida na itachukua muda gani kuwa na faida?
e. Nini matarajio yako ya mapato na matumizi kwa miaka 4 ya kazi (ni mapato na matumizi kiasi gani katika mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, wa tatu na wa nne)?

f.  Unahitaji mtaji wa kiasi gani (kiasi gani cha fedha unachohitaji kuwekeza) katika mwaka wa kwanza,wa pili, wa tatu na wa nne ili kuendesha biashara yako?
g. Utawezaje kupata kiasi hicho cha mtaji? Je ni kwa kuanza kuweka akiba katika benki au kuomba mkopo na kwa gharama gani?. Je mchango wako katika mtaji ni kiasi gani?
h. Je mradi wako unaweza ukabeba gharama zinazotakiwa kiundeshaji na bado ukazalisha faida?

5. Uzoefu  wako  katika  ujasiriamali na uwajibikaji.

a. Tathmini kiwango chako cha elimu na uzoefu wako unaohusiana  na wazo lako la biashara na mahusiano uliyo nayo na wadau muhimu ki- sekta wewe kama mjasiriamali.
b. Tathmini kuhusu wataalam wa fani mbalimbali ambao utahitaji kuwatumia katika maeneo ambayo wewe si mtaalam wala mzoefu ili kufanikisha uanzishaji na uendeshaji wa biashara yako.
c. Kwa ufupi tathmini nia/malengo yako ya kutimiliza kuanza na kukua kwa biashara ukizingatia muda utakaotumia kupanga, muda unaokusudia kutumia katika mradi, kiwango cha fedha za kwako mwenyewe unachoridhia kuweka katika mradi n.k.

Z I N G A T I A  H A Y A  A N D A A  T U O N E


ili  ndoto  yako  ya  kumiliki  na  kuendesha  biashara  endelevu  itimie


Azania Bank Limited Masdo House Samora Avenue
Box 9271Dar es Salaam, Tanzania
Tel: 255 22 2118014, 2117998 - 9, 2118025 - 6
Fax 255 22 2118010 - 1 www.azaniabank.co.tz