Saturday, June 15, 2013

Ndege maalumu za kivita kutawala anga Dar

Pamoja na ulinzi wa hali ya juu ardhini, ndege za kivita zitatawala anga ya Tanzania kwa saa 24 kwa siku zote atakazokaa.


Dar es Salaam. Idara ya Ujasusi ya Marekani imeweka bayana kwamba inajitegemea kwa ulinzi katika ziara nzima ya Rais Barack Obama kwa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senegal.
Kwa mujibu wa taarifa ya idara hiyo, katika kuhakikisha usalama wa kutosha wakati wa ziara ya Obama tayari maofisa wao wameshakamilisha maandalizi ya kiusalama katika nchi zote anazotarajiwa kutembelea.
Meli ya kivita kutua bandarini
Katika kuchukua hatua hizo, meli kubwa kabisa ya kivita yenye hospitali maalum zipo tayari kwa ya kambi maalumu katika bandari maalum za nchi atakazotembelea, kwa ajili ya kukabiliana na dharura yoyote ya kiafya ya Obama na familia yake.
Ili kuwawezesha maofisa wa kijasusi wa Marekani, ndege ya kijeshi ndiyo itakayobeba magari 56 zikiwemo limousine 14 na magari matatu maalumu ya kubeba mizigo.
Malori hayo yatakuwa yakibeba vioo ambavyo ni vizuizi maalumu vya risasi na milipuko kwa ajili ya kuongeza ulinzi kwenye hoteli atakazolala yeye na familia yake.
Ndege za kivita kutawala anga
Ndege za kivita zitakuwa zikiruka kwa zamu wakati wote muda wa sasa 24 kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi katika sehemu atakayokuwa Rais Obama na kudhibiti anga yote kwa wakati huo dhidi ya ndege yoyote ngeni itakatosogea usawa wao.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwananchi, hakuna Maandalizi ya safari hiyo ambayo tayari yamekamilika yanapolinganishwa na safari nyingine za aina hiyo zilizowahi kufanyika, waraka maalumu kuhusu suala la usalama unaonesha kwamba kumekuwa na juhudi za ziada zakuhakikisha ulinzi wa Amiri jeshi huyo Mkuu wa Marekani akiwa nje ya nchi.
Kabla ya safari yake kwa nchi za Afrika, Obama atatembelea Ireland na Ujerumani ikiwa ni sehemu ya kuongeza changamoto inayokabili masuala ya usalama wake.
Lakini zaidi, safari ya Obama kwa nchi za Afrika inadhaniwa kuwa inayolazimisha waandaaji kuwa na umakini wa hali ya juu na kuifanya iwe aghali zaidi katika utawala wa Obama kuliko ziara katika nchi za ulaya, kwa mujibu wa wataalamu wa mipango.
Familia ya rais huyo inatarajiwa kutembelea nchi tatu za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senagal kuanzia Juni 26 hadi Julai 3 mwaka huu.


No comments:

Post a Comment