Thursday, May 16, 2013

Baadhi yaNjia Unazoweza Kutumia Kupata wazo Bora kabisa la Biashara


Wazo laBiashara ni moja ya mambo yanayowaumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ilikuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii  nzima,

HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA

1. TUMIA UJUZI ULIONAO
Ujuzi  ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupatawazo la Biashara, Mfano kama wewe umeajiliwa nani mtaalamu wa ramani, kwanini usianzishe na wewe kitengo cha biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni kuchapisha vitabu kwanini usianzishe kiwanda kidogo cha kuchapisha vitabu cha kwako?
Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza naya kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasiliamali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazofanya nakwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe.



2. BADILISHA HOBY YAKO KUWA PESA

Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu hujakutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwanini usianze hiyo biashara ya kufugambwa?
Kama Hobby yakoni Kuogelea, kwanini usinzishe mabwawa yakuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?
Kama unapenda gardening unaweza anza biashara yakufanya landscape gardening


3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYALI IPO
Ukishindwa kabisa kupata wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtumwingine nakuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali   kwahiyo unaweza nunua na kuendeleanayo.


4. Kununua Franchise
Hii ni moja ya njia zinazotumika kwa sasa na sehemu nyingi  sana, Unawezanunua Popular Brand nakuifanyiakazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoahuduma sawa na Brandi yenyewe, na hii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE
Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapaTaarifa maana inaweza kukuingiza hatarini na ukajikuta unafilisiwa,
Na ilishawahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, sijui walimalizana vipi.


5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta wanakubalika katika jamii mfano mcheshi sana au bingwa wa kusuruhisha migogoro n.k, unaweza kutumia hicho kipaji au karama yako kufanyabiashara katika eneo unalokaa maana itakusaidia kupata wateja wengi.

6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani na geuza kitu hicho  kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenu au maeneo unayoenda kustalehe
-Ni kitu gani huwakinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazoni za muhimu?
-Ni bidhaazipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirani huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?


7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, kwa hiyo unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyiakazi.


8. TUMIA TECHINOLOGIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyotumika kwa sasa na vinavyotumiwa na watu wengi, kwa hiyo mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara


9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI ZINGINE WANAHITAJI NINI
Unaweza tumia uwepo wa makampuni fulani au taasisi fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi n.k, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi.


10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza


11. ANAGALIA NEWS NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala nzuri sana za uchumi na biashara, hata TBC huwa ina makala fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku hizi kazi yao ni hiyo tu, nikuonyesha ubunifu wa wajasirimali, kwahiyo TV, radio na magazeti yanaweza toamchango wa kutosha kwa wewe kupatawazo la biashara.


12. NUKUU BIASHARA NA  MAWAZO AMBAYO YAMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazotumika kwa sasa, unaweza nukuu kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuyafanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika.


13. TUMIA NJIZA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA biashara- maonyeshoyabiashara
-Magazeti,
- Kwenye taasisi za umma zinazohusika na biashara
-Kwa marafiki


14. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyofanya wakina Thomas Edson, Michael Dell nawengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako.


SO HIZO NI MOJA YA NJIA ZA KUTUMIA, INGAWA BADO KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUFANYA ILI KUOATA WAZO LA BIASHARA LILILO BORA


No comments:

Post a Comment