Wednesday, January 8, 2014

RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE KWA CHADEMA

*Nyaraka hii imechomolewa kwa siri toka Chadema makao makuu

RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE KWA CHADEMA

UCHUNGUZI WA MWENENDO WA KISIASA WA ZITTO Z. KABWE NDANI NA NJE YA CHADEMA.


UTANGULIZI:
Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa anakisaliti chama.
Hilo liliilazimu timu ya kijasusi ya chama kuanza kufuatilia nyendo zake kwa ukaribu zaidi usiku na mchana ili kujiridhisha pasipo kuacha chembe ya mashaka. Ifahamike kuwa chama kina idara ya ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake yenye uwezo wa kufuatilia nyendo za majasusi wa nje na viongozi na wanachama wake popote walipo kwa masaa 24. Baada ya kujiridhisha kuwa mwenendo wake ni wa mashaka, bila kusita timu ya ujasusi ilianza kazi rasmi ya ujasusi dhidi ya nyendo zote za Zitto Zuberi Kabwe


MAMBO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI DHIDI YA ZITTO KABWE.

Kumfuatilia yeye binafsi nyendo zake.
Kufuatilia mawasiliano yake ya simu.
Kufuatilia mawasiliano yake ya barua pepe.
Kufuatilia pato lake nje ya kazi zake halali za kibunge.

SEHEMU YA KWANZA 2008

Chombo chetu cha ujasusi tulichokipandikiza kwa siri katika nyendo zote za Zitto Kabwe na ndani ya vikao vya mwanzo kabisa vya Zitto na viongozi serikalini, nahata vile vikao muhimu vya idara ya ujasusi ya chama cha mapinduzi (ccm), kinatupa fursa ya kuweka msingi wa kuimarisha chama cha CHADEMA na kutenda haki kidemokrasia kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla:

Mnamo Jumatatu ya tarehe 16/6/2008 saa 09:46 asubuhi, Mh Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba +255754787550 alipokea simu kutoka kwa Ramadhani Ighondu mwenye namba +255717760473 ambaye ni afisa Usalama wa Taifa anayefanya kazi ikulu hivi sasa. Alijitambulisha kuwa yeye ni Usalama wa Taifa ametumwa na mkuu wake wa kazi aje aongee na Zitto, Maelezo ya msingi katika simu hii ilikuwa ni bwana Ramadhani Ighondu kuomba miadi ya kuonana kutokana na agizo la mkuu wake wa kazi.

Siku sita baadae yaani Jumatatu ya tarehe 23/6/2008 saa 07:52 asubuhi, Zitto alipigiwa tena simu na Ramadhani Ighondu akimkumbusha maongezi yao waliyo fanya siku 6 zilizopita na kumuomba siku hiyo jioni waonane, ingawa Zitto alionekana kusita kidogo lakini baadae alikubali, Walikubaliana wakutane Sea Cliff Hotel, ilipofika jioni ya siku hiyo Zitto akiwa na marafiki zake wawili Omar Lyasa na Abdalah Said walifika Sea Cliff Hotel wakaketi na kuagiza vinywaji, Baada ya kama dakika kumi hivi Zitto alipokea simu ikimuelekeza alipo bwana Ramadhani Ighondu kisha Zitto akawaambia marafiki zake wamsubiri kidogo, akaondoka kuelekea aliko elekezwa…..

Mashariki mwa lango kuu la kuingilia Sea Cliff Hotel mita kama tatu tu kuna mlango mdogo unaoelekea kwenye vyumba maalumu (VIP), chumba namba 8 ndicho Zitto alichokuwa anaelekezwa kwa simu kuingia, chumba hiki kina meza moja na sofa zilizo zunguka meza ile zenye uwezo wakukaliwa na watu watano hadi sita, Ndani ya chumba kile Zitto anakutana na watu watatu ambao ni Steven Wasira, Ramadhani Ighondu na Abdalla Punja (hawa wote ni TISS)